GST YAWEKEZA UJUZI, TEKNOLOJIA KUBORESHA TAFITI ZA MADINI NCHINI
GST YAWEKEZA UJUZI, TEKNOLOJIA KUBORESHA TAFITI ZA MADINI NCHINI
Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa GST, Neema Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la GST katika Maonesho ya Kilimo ya Kimatiafa Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela ,Nzuguni jijini Dodoma, Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imesema inaendelea kuwekeza katika mafunzo na ushirikiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha uwezo wa kitaalamu katika tafiti za jiosayansi na uchunguzi wa sampuli maabara. Akizungumza wakati wa ziara katika Banda la GST kwenye Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa GST, Neema Mhagama, amesema taasisi hiyo imekuwa ikiwajengea uwezo watumishi wake kupitia mafunzo na ushirikiano wa kitaalamu na taasisi za ndani na nje ya nchi Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha GST inaendelea kuendana na…