Global Education Link Yaunga Mkono Dira ya Rais Samia
Global Education Link Yaunga Mkono Dira ya Rais Samia
Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link mwaka 2026. Wanafunzi hao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, afya, sheria na biashara. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa. “Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tunatarajia wanafunzi 198 kwenda kusoma nchini India. Hili si kundi la mwisho kwa sababu bado tuna wanafunzi wengine wanaoendelea kukamilisha taratibu zao,” am…