FEDHA ZA CSR ZA BARRICK NORTH MARA ZAENDELEA KUFANIKISHA MIRADI YA KUBORESHA ELIMU TARIME
FEDHA ZA CSR ZA BARRICK NORTH MARA ZAENDELEA KUFANIKISHA MIRADI YA KUBORESHA ELIMU TARIME
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akiongozwa na Mwalimu Charles Gibiti kukagua jengo hilo. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa pili kulia), akifurahi kuzindua mradi wa jengo la utawala la Shule ya Sekondari Mjini Kati uliotekelezwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoka mgodi wa Barrick North Mara. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele na viongozi wengine wa wilaya. Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi na wafanyakazi wenzake akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Tarime mara baada ya uzinduzi wa ofisi ya utawala katika Shule ya Sekondari ya Mjini kati Kupitia utekelezaji wa mkakati endelevu wa kampuni na sera za serikali kwa weledi, mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime unaendelea kufanikisha miradi mbalimbali kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR), hususani katika sekta ya afya na elimu katika vijiji vinavyozunguka mgodi. Miradi inayotekelezwa kwa kut…