DKT. MWIGULU: TUBORESHE VIWANGO KWENYE BIDHAA
WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa wazalishiaji mbalimbali nchini waboreshe bidhaa zao ili zimudu ushindani wa kimataifa na ziweze kushindana kila siku na siyo wakati wa maonesho tu. “Bidhaa ambazo tuko nazo zisiwe kwa ajili ya maonesho, bali ndiyo iwe standard ya bidhaa zetu katika maisha yetu. Tukishafikia hatua hiyo, tutakuwa tumetatua mambo mengi kwa mpigo ikiwemo kujihakikishia kwamba bidhaa zetu zinapata soko, ni lazima tuendelee kuoanisha uzalishaji na vigezo vya kimataifa vya masoko,” amesema. Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti Mosi, 2026) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane), yaliyofunguliwa rasmi katika Viwanja vya Dkt. John John S. Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma. Amesema kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zinazozalishwa kupata masoko popote duniani kutokana na ubora utakaokuwa nazo. “Tutengeneze bidhaa zetu za kila siku kama vile za kwenda kwenye maonesho. Katika maeneo meng…