DKT. MIGULU NCHEMBA ATATUA MGOGORO MWINGINE WA ARDHI
DKT. MIGULU NCHEMBA ATATUA MGOGORO MWINGINE WA ARDHI Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 15, 2026 ameendelea kutatua kwa njia ya maridhiano migogoro sugu inayowakabili wananchi na mara hii ametatua mgogoro wa ardhi kati ya Bi. Alia Shariff na Bi Devotha Delfina Elisei uliodumu miaka 28 katika eneo la Goba jijini Dar es salaam . Bi. Alia Shariff, mkazi wa Dar es Salaam, alimwandikia barua Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 20 Januari 2026, akiomba amsaidie kutatua mgogoro huo na katika barua hiyo, alieleza kuwa eneo analolalamikia limemilikiwa na wanae tangu mwaka 1998 na kwa muda wote huo ametafuta suluhu ya jambo hilo bila mafanikio. Waziri Mkuu alituma Timu ya Watalaam kutoka Ofisini kwake ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu – Mahusiano, Asasi za Kiraia na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Bw. Tryphone Mkolokoti, na Katibu wake ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu – Masuala ya Ardhi, Bw. Senso Magessa ambayo ilishirikiana na Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es salaam, Shukuruni Kyando, Watalaam wa Ar…