BUNAZI GREEN ACRES YAONGOZA KITAALUMA MIAKA 10 MFULULIZO
BUNAZI GREEN ACRES YAONGOZA KITAALUMA MIAKA 10 MFULULIZO
Na Mwandishi Wetu SERIKALI imezitaka shule nchini kuweka kipaumbele kwenye mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wanafunzi wao ili kwenda sanjari na dunia ya sasa ya utandawazi na teknolojia inayokua kwa kasi. Imesema teknolojia inakwenda kwa kasi kubwa hivyo shule zinapaswa kuwa na miundombinu bora ya wanafunzi kujifunza TEHAMA, huku ikiipongeza shule ya Bunazi Green Acres iliyoko mji mdogo wa Bunazi, Kata ya Kassambya, wilayani Missenyi, kwa kuwa mfano kwenye eneo la mafunzo ya TEHAMA. Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, Phocus Rwegasira, wakati wa mahafali ya 10 ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo, ambapo alikuwa mgeni rasmi. Alisisitiza kuwa mafunzo ya teknolojia ni muhimu kwani dunia inakwenda kwa kasi kwenye eneo hilo, huku akisisitiza pia umuhimu wa ushirikiano kati ya wazazi, walimu na jamii katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na malezi yanayowaandaa kuwa viongozi na wataal…