Breaking : DKT. EMMANUEL NCHIMBI AFUKUZWA CCM, NDEJEMBI APENDEKEZWA MAKAMU WA RAIS
Breaking : DKT. EMMANUEL NCHIMBI AFUKUZWA CCM, NDEJEMBI APENDEKEZWA MAKAMU WA RAIS
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemvua uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi, katika uamuzi uliofikiwa Jumatano, Agosti 26, 2026, siku moja baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu shughuli za kisiasa. Uamuzi huo umetangazwa usiku wa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Dk. Migiro amesema Halmashauri Kuu ilipitia taarifa mbalimbali zilizokuwepo pamoja na Katiba ya CCM na kufikia uamuzi wa kumvua uanachama Dk. Nchimbi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa maadili. “Baada ya kupitia taarifa zote zilizokuwepo, Katiba za CCM, kwa kauli moja Halmashauri Kuu imefikia uamuzi kwamba, kutokana na ukiukwaji wa maadili, afukuzwe uanachama na CCM imefikia uamuzi huo. Si mwanachama wa CCM tena,” amesema Dk. Migiro. NCHIMBI ALIOMBA KUJIUZULU Uamuzi huo umefanyika siku moja baada ya Dk. Nchimbi kumwandikia Rais…