BMT LAIPA HEKO BAOBAB KUKUZA MICHEZO KWA WANAFUNZI
BMT LAIPA HEKO BAOBAB KUKUZA MICHEZO KWA WANAFUNZI Na Victor Masangu, Bagamoyo Baraza la michezo la Taifa (BMT) limeipongeza kwa dhati Taasisi ya Shajar inayomiliki shule ya Baobab kwa kuweza mipango madhubutti katika kukuza sekta ya michezo mbali mbali kwa wanafunzi na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiana na sapoti ya hali na mali katika kuendeleza maono waliyonayo katika kukuza vijapi vya watoto hasa wakiwa mashuleni. Kauli hiyo imetolewa na Afisa michezo mwandamizi wa (BMT) Charles Maguzu wakati wa sherehe za miaka 20 ya Baobab ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi mbali mbali kwa washindi walioweza kuibuka kidedea katika michezo mbali mbali ikiwemo, mchezo wa soka, riadha, pete, pamoja na michezo mingine ambapo washindi walizawadiwa vikombe pamoja na medali. Mwandamizi huyo amesema kwamba wao kama serikali kupitia baraza hilo wataendelea kushirikiana bega kwa bega na uongozi wa shule hiyo katika kukuza vipaji mbali mbali walivyonavyo wanafunzi wa shule hiyo kwani kwa lengo la kuweza kuwaendeleza zaidi kufika mbali. Kadh…