BILIONI 50 ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA HUDUMA ZA SARATANI TANZANIA
BILIONI 50 ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA HUDUMA ZA SARATANI TANZANIA
Na Dotto Kwilasa, Dodoma WAGONJWA wa saratani nchini huenda wakaanza kusubiri kwa muda mfupi zaidi kupata huduma za matibabu, huku safari za kufuata huduma hizo Dar es Salaam zikitarajiwa kupungua, baada ya Serikali kuelekeza zaidi ya Sh bilioni 50 katika miundombinu, vifaa tiba na teknolojia za kisasa za saratani. Uwekezaji huo umehusisha ujenzi wa vituo vipya, ununuzi wa mashine za kisasa za tiba ya mionzi na uchunguzi, uboreshaji wa maabara pamoja na kuimarisha uwezo wa wataalamu, hatua inayolenga kuongeza wigo wa huduma na kuzifikisha karibu zaidi na wananchi. Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa Kituo cha Saratani Mbeya wenye thamani ya Sh bilioni 11, ambao umefikia asilimia 57 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027 kabla ya kuanza kutoa huduma Julai mwaka huo. Amesema kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia wananchi wa Mbey…