ALAYA ANAYEWANIA GUINNESS WORLD RECORDS APOKELEWA TANZANIA
ALAYA ANAYEWANIA GUINNESS WORLD RECORDS APOKELEWA TANZANIA
Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Tanzania Safari Channel, imemkaribisha na kumpokea nchini Tanzania mhamasishaji wa amani duniani na mpiga hatua wa kimataifa, Saddam Suleiman Ali Alaya, anayetekeleza safari ya kihistoria ya The World’s Longest Peace Walk. Saddam ameingia nchini kupitia Mpaka wa Kasesya uliopo Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, akianzia rasmi hatua ya safari yake ya takribani siku 35 nchini Tanzania. Katika kipindi hicho atapita katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma kabla ya kuondoka kupitia Mpaka wa Manyovu, akiwa na dhamira ya kuhamasisha amani, mshikamano wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kama moja ya vivutio bora vya utalii duniani. Safari hiyo sehemu ya mradi wa kimataifa unaolenga kutembea zaidi ya kilomita 23,000 kutoka Cape Town, Afrika Kusini hadi Magadan, Urusi, kupitia nchi 18 kati ya mwaka 2026 na 2028. Tanzania ni…