Airtel Money School Pay Yarahisisha Ulipaji Ada, Shule Zaidi ya 800 Zajiunga Tanzania.

Airtel Money School Pay Yarahisisha Ulipaji Ada, Shule Zaidi ya 800 Zajiunga Tanzania.
HUDUMA  ya Airtel Money School Pay imeendelea kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa ada za wanafunzi nchini, huku shule zaidi ya 800 kutoka mikoa 16 zikiwa tayari zimejiunga na kutumia mfumo huo wa kidigitali unaolenga kurahisisha malipo kwa wazazi na uendeshaji wa kifedha kwa shule. Akizungumza wakati wa ziara katika Salaam Pre and Primary School, iliyopo Chamazi, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Afisa Huduma wa Airtel Money School Pay, Roda William Mganga, alisema huduma hiyo ilianzishwa mwaka 2024 ikiwa na lengo la kutoa njia rahisi, salama na yenye ufanisi katika ulipaji wa ada na usimamizi wa taarifa za malipo. Mganga alisema tangu kuanzishwa kwake, School Pay imefanikiwa kufikia shule zaidi ya 800 katika mikoa 16 nchini, huku lengo likiwa ni kuunganisha shule 1,000 kila mwaka. Mikoa ambayo tayari imefikiwa na huduma hiyo ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza na Mtwara. Alisema miongoni mwa shule zinazotumia mfumo huo ni pamoja na St. Anne M…