Airtel Fursa Lab yarudi kwa sura mpya, vijana kunufaika na elimu ya kidijitali
Airtel Fursa Lab yarudi kwa sura mpya, vijana kunufaika na elimu ya kidijitali
Dar es Salaam. WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Kijitonyama sasa wana nafasi zaidi ya kujifunza, kufanya majaribio na kuendeleza ubunifu wa kiteknolojia baada ya Airtel Africa Foundation kuzindua upya jengo la Airtel Fursa Lab lililokarabatiwa. Airtel Fursa Lab, iliyoanzishwa mwaka 2020 kwa ushirikiano kati ya Airtel Africa Foundation na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), imekuwa kituo cha kujifunzia na kukuza ujuzi wa kidijitali kwa wanafunzi, walimu na vijana kutoka ndani na nje ya jamii inayozunguka shule hiyo. Ukarabati wa jengo la Airtel Fursa Lab umeongeza mazingira ya kujifunzia na kufanya majaribio, huku kituo hicho kikilenga kuwawezesha vijana kutumia teknolojia kwa ajili ya kujifunza na kubuni suluhisho za changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku. Tangu kuanzishwa kwake, zaidi ya watu 5,800 wamenufaika na Fursa Lab, wakiwemo wanafunzi, walimu, vijana, wajasiriamali na wanawake. Kituo hicho pia kimekuwa kikitoa fursa kwa wanafunzi waliomaliza Darasa la Saba, K…