AGA KHAN UNIVERSITY YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MUSTAKABALI WA UANDAAJI WALIMU
AGA KHAN UNIVERSITY YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MUSTAKABALI WA UANDAAJI WALIMU
Na Avila Kakingo CHUO Kikuu cha Aga Khan kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Afrika Mashariki (IED, EA), kimewakutanisha waelimishaji wa walimu, watunga sera, watafiti, viongozi wa shule, washirika wa maendeleo, walimu wanafunzi na wataalamu wa elimu kutoka Afrika Mashariki na maeneo mengine kujadili mustakabali wa uandaaji wa walimu. Mkutano huo wenye kaulimbiu “Kufikiria Upya Uandaaji wa Walimu: Mabadilishano ya Kujifunza Afrika Mashariki kuhusu Ubunifu na Utendaji”, unalenga kutoa jukwaa la kubadilishana uzoefu, kuchunguza mbinu bunifu na kuandaa kwa pamoja suluhisho la kuimarisha uandaaji wa walimu. Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa IED, EA, Profesa Jane Rarieya, amesema mustakabali wa elimu katika Afrika Mashariki hautegemei kuwa na walimu wa kutosha pekee, bali namna wanavyoandaliwa, kusaidiwa na kuwezeshwa katika taaluma zao. Profesa Rarieya amesema mabadiliko ya elimu yanachochewa na matumizi ya teknolojia za kidijitali na akili bandia (AI), mabadiliko ya tabianchi, ongez…