WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA MBINGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Joseph Kashushura,akizungumza na baadhi ya watumishi wa kituo kipya cha afya Langiro baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo hicho,katikati aliyevaa miwani ni Katibu wa afya wa Halmashauri George Mhina na kulia Mhandisi wa ujenzi Neema Mbilinyi. Na Mwandishi Maalum, Mbinga WATUMISHI wa afya Halmashauri ya wilaya Mbinga,wamewatakiwa kuzingatia maadili,weledi,kutoa huduma bora na huruma kwa wagonjwa ili wananchi wavutiwe kwenda kutibiwa kwenye vituo vya afya na hospitali zinazojengwa na Serikali. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura,wakati akizungumza na watumishi wapya wa kituo cha afya Langiro kata ya Langiro baada ya kukagua ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo hicho. Amewataka,kujipanga kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili hospitali na vituo vya umma viwe sehemu ya kimbilio,ndiyo maana Serikali imeendelea kuajiri wataalamu wenye sifa w…