VIJANA WA RUVUMA KUNUFAIKA NA AJIRA ZA MRADI WA BARABARA YA SONGEA-LUTUKIRA

VIJANA WA RUVUMA KUNUFAIKA NA AJIRA ZA MRADI WA BARABARA YA SONGEA-LUTUKIRA
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdallah Ulega akizungumza na wakazi wa mkoa wa Ruvuma leo juni 1 2026 alipowasili katika hafla ya utambulisho wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Songea-lutukira yenye kilomita 100 na -Songea Bypass yenye kilomita 16 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed akizungumza katika hafla ya utambulisho wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Songea-lutukira yenye kilomita 100 na Songea Bypass yenye kilomita 16  Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma. Serikali imeagiza vijana wa mkoa wa Ruvuma kupewa kipaumbele katika ajira zitakazotokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Songea–Lutukila yenye urefu wa kilomita 100 pamoja na barabara ya mchepuko ya Songea Bypass yenye kilomita 16.  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdallah Ulega, wakati wa hafla ya utambulisho wa mradi huo mkubwa wa kimkakati uliofanyika mkoani Ruvuma. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Ulega amesema serikali inataka wananchi wa Ruvuma wanufaike moja kwa moja …