UHIFADHI WA MIKOKO WAPEWA MSUKUMO MPYA TANGA

UHIFADHI WA MIKOKO WAPEWA MSUKUMO MPYA TANGA
Na Oscar Assenga,TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amewataka wananchi kuacha ukataji holela wa mikoko na kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wake, akisema misitu hiyo ni muhimu kwa kulinda fukwe, kuhifadhi viumbe wa majini na kuimarisha uchumi wa jamii za pwani. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, ameitaka jamii kuachana na tabia ya ukataji holela wa miti ya mikoko katika maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi, akionya kuwa endapo vitendo hivyo vitaendelea vinaweza kuhatarisha makazi ya viumbe wa majini, maisha ya wananchi wanaotegemea rasilimali za bahari pamoja na usalama wa fukwe. Dkt. Burian alitoa kauli hiyo Juni 28 wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Uhifadhi wa Ikolojia ya Mikoko yaliyofanyika katika eneo la Donge Mnyanjani, Jijini Tanga. Alisema Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na ukanda mpana wa pwani pamoja na misitu ya mikoko yenye umuhimu mkubwa wa kiikolojia na kiuchumi katika wilaya za Mkinga, Pangani, Muheza na Jiji la Tanga. Aliele…