TUTUBA: THAMANI YA FEDHA KUBAKI IMARA KUELEKEA KIPINDI CHA MAVUNO
TUTUBA: THAMANI YA FEDHA KUBAKI IMARA KUELEKEA KIPINDI CHA MAVUNO
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amesema thamani ya fedha itaendelea kuwa imara kuelekea kipindi cha mavuno ili kuwawezesha wakulima kupata thamani stahiki ya mazao yao kulingana na shughuli za kiuchumi wanazozifanya. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Julai 10, 2026, Tutuba amesema kiwango cha riba ya Benki Kuu cha asilimia 6.25 kinalenga kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa bei na mfumuko wa bei unaendelea kubaki kati ya asilimia 3 hadi 5. Amesema kiwango hicho pia kitawezesha Mabenki kuwa na ukwasi wa kutosha kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wananchi na wafanyabiashara, hivyo kusaidia shughuli mbalimbali za uzalishaji na biashara nchini. Tutuba amesema wakulima wanapoanza kuvuna mazao yao, thamani imara ya fedha itasaidia kuhakikisha wanapata malipo yanayolingana na thamani halisi ya mazao yao sokoni. Ameongeza kuwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi pia watanufaika kwa kupata…