Posts

TPSC YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUFANYA TAFITI TUMIZI ZA KUBORESHA UTENDAJI WA SERIKALI

TPSC YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUFANYA TAFITI TUMIZI ZA KUBORESHA UTENDAJI WA SERIKALI
Dar es Salaam, Julai 3, 2026  Serikali imekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafanikio makubwa ya kupanua huduma zake nchini, hatua iliyowezesha kuongeza fursa za mafunzo kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia ongezeko la kampasi kutoka mbili hadi sita katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete, wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya TPSC yaliyofanyika katika Julius Nyerere International Convention Centre. "Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, Chuo hiki kimepitia hatua kubwa za maendeleo. Kutoka kampasi mbili wakati wa kuanzishwa kwake hadi kufikia kampasi sita leo; kutoka programu chache za mafunzo hadi kuwa taasisi inayotoa mafunzo ya muda mfupi, programu za muda mrefu, mafunzo kwa njia ya mtandao, tafiti tumizi na shauri za kitaalamu," alisema Kikwete. Alisema maendeleo hayo yanaonesha dhamira ya TPSC ya kuhakikisha…