TEA YAHIMIZWA KUDUMISHA KASI YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

TEA YAHIMIZWA KUDUMISHA KASI YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM MKURUGENZI wa Idara ya Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima Zanzibar, Mashavu Ahmada Fakih, ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya elimu nchini, huku akiwataka wadau wa maendeleo na wananchi kuendelea kuchangia Mfuko wa Elimu ili kuongeza ubora wa elimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Akizungumza leo Julai 11, 2026 katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mashavu amesema TEA imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake ya elimu bila kujali mahali anapoishi. Amesema mamlaka hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu ya elimu Tanzania Bara na Zanzibar kupitia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya shule pamoja na taasisi mbalimbali za elimu, hatua ambayo imeongeza mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Amebainisha kuwa mchango wa TEA umekuwa muhimu zaidi katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kut…