St Anne Marie Academy Yaahidi Kuendelea Kusomesha Waliofiwa Na Wazazi
St Anne Marie Academy Yaahidi Kuendelea Kusomesha Waliofiwa Na Wazazi
Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amewataka wakaguzi wa shule kutenda haki kwa shule binafsi na kuziona kama mshirika wa maendeleo badala ya mshindani. Kadhalika, Profesa Tibaijuka ameipongeza shule ya St Anne Marie Academy kwa kuendelea kusomesha bure wanafunzi wanaofiwa na wazazi wao ikiwa shule pekee ya binafsi inayofanya hivyo kwa sasa nchini. Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa shule hiyo Julai 18, mwaka 2001. Aliwataka wakaguzi wa elimu nchini kuacha kuziwekea vikwazo shule binafsi kwa kuziona kama washindani kwenye sekta ya elimu na badala yake wanatakiwa kuwaona kama washirika muhimu kwenye kutoa huduma hiyo. ”Unakuta wanawawekea wenye shule binafsi viwango vya kusadikika tofauti kabisa na shule za umma, sisemi kwama muwawekee viwango hafifu, hapana mimi nataka uwiano wa haki baina ya shule za umma na shule binafsi,” alisema Alisema shule zing…