SGR Yafikia Asilimia 98, Usafirishaji wa Mizigo Dar–Bahi Waongezeka
SGR Yafikia Asilimia 98, Usafirishaji wa Mizigo Dar–Bahi Waongezeka
Na Sheila Ahmadi, Bahi Serikali inaendelea kuboresha Huduma za usafirishaji wa Reli ya Mizigo kutoka Dare salaam hadi Bahi ikiwa imefikia asilimia 98 ya utekelezaji. Akizungumza Mkoani Dodoma na wanahabari kwenye stesheni ya Mizigo bahi Mhandisi wa mradi wa kipande cha pili cha stesheni ya SGR ya mizigo kutoka Dar es salaam hadi Makutupora Christina Samweli amesema kufikia sasa mradi wetu uko Mwishoni kukamilika huku Mkandarasi akiwa amefikia asilimia 98% hivyo tunaanza kuendesha treni ya mizigo kutoka Daresalaam hadi kufika Bahi mkoani Dodoma. Tumeanza kusafirisha Mizigo kutoka kwenye Bandari ya Dar es salaam hadi Stesheni ya Bahi ambapo ina uwezo wa kupokea Makasha 1500 kwa Wakati Mmoja huku tukisafirisha kwa SGR na kuhamishia kwenye Reli ya Zamani MGR kwenda Mwanza,Isaka na Kigoma. "Nitoe wito kwa wadau Wote nchini wanaosafirisha mizigo watumie usafiri wa reli kwani usafiri wa Reli ni Waharaka na salama Zaidi ambapo unatumia muda mchache wa masaa Matano kwenye kusafir…