Sekretarieti ya Maadili: Hatuna Ugomvi na Viongozi Matajiri Waliopata Utajiri Halali

Sekretarieti ya Maadili: Hatuna Ugomvi na Viongozi Matajiri Waliopata Utajiri Halali
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam OFISI ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema haina tatizo na viongozi wa umma wenye utajiri, ilimradi mali walizonazo zimepatikana kwa njia halali bila kutumia vibaya madaraka yao au kufanya biashara zinazokinzana na nafasi wanazoshikilia serikalini. Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo, Honoratus Ishengoma, wakati akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ishengoma alisema viongozi wa umma wanatakiwa kuzingatia masharti ya kimaadili yaliyowekwa na sheria, ikiwemo wajibu wa kutangaza mali na madeni yao pamoja na kueleza vyanzo vya mapato yao ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Amesema kuwa lengo la ushiriki wa Sekretarieti katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu…