RAS ARUSHA ASISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA WATENDAJI WA SERIKALI KATIKA MKOA HUO

RAS ARUSHA ASISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA WATENDAJI WA SERIKALI KATIKA MKOA HUO
Asema umoja, ushirikiano, upendo na uelewa wa pamoja utatimiza adhma ya Serikali na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Na Mwandishi Maalumu Arusha  Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila amewasisitiza watendaji wa Serikali katika mkoa huo, kuanzia Sekretarieti ya Mkoa, halmashauri na Taasisi na Mashirika yote ya Umma, kufanya kazi kwa ushirikiano kisekta ili kutimiza adhma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.  Dkt. Nguvila ametoa rai hiyo,  wakati akifungua kikao kazi cha robo ya mwisho,  kilichowakutanisha Watendaji wa Serikali wa mkoa huo kutathmini utendaji wa shughuli wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Masai Land wilaya ya Arumeru leo Julai 17,2026. “Lengo la kikao kazi hiki ni kutathmini utendaji wa shughuli za Serikali kwa Mkoa, kuona mafanikio na kubaini changamoto zilizojitokeza, utakaotoa dira na mwelekeo wa utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa mwaka mpya wa fedha wa 2026/27, kukiwa na mipan…