RAIS MWINYI ATOA MILIONI 200 KUSAIDIA KITUO CHA IRSHAAD LUSHOTO, ARIDHIA OMBI LA PROF. SHEMDOE
RAIS MWINYI ATOA MILIONI 200 KUSAIDIA KITUO CHA IRSHAAD LUSHOTO, ARIDHIA OMBI LA PROF. SHEMDOE Na OWM – TAMISEMI, Lushoto Mhe. Alhaji Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, amekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa kutoa mchango wa Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya kuendeleza Kituo cha Elimu ya Kiislamu Irshaad (Irshaad Islamic Centre) kilichopo Lushoto, mkoani Tanga. Fedha hizo zinatarajiwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kituo hicho, ikiwemo kuboresha Chuo cha Ufundi, kuanzisha bustani ya kisasa, kujenga madrasa yenye kukidhi mahitaji ya wanafunzi, kujenga nyumba za walimu, jengo la kupokelea wageni, hospitali pamoja na ukumbi wa kisasa wa kufanyia shughuli mbalimbali za kielimu na kijamii. Prof. Shemdoe alitoa ombi hilo Julai 5, 2026 wakati wa Sherehe ya Maulidi ya Kumswalia Mtume Muhammad S.A.W iliyoandaliwa na Sheikh Sharrif Hussein Ahmad Badawiyy wa Kituo cha Irshaa…