RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo, tarehe 18 Julai 2026, ameendelea na ziara yake ya kikazi nchini India kwa kutembelea Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Taasisi ya Teknolojia ya India Madras (IIT Madras), jijini Chennai. Kituo hicho kinawaunganisha wanataaluma, watafiti, wanafunzi, mampuni na wajasiriamali katika kubuni na kuendeleza teknolojia zinazolenga kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Akiwa katika kituo hicho, Rais Dkt. Mwinyi ameongozwa na Mkuu wa IIT Madras, Prof. V. Kamakoti, pamoja na viongozi na wataalamu wa taasisi hiyo, ambao wamemweleza kuhusu tafiti, shughuli na programu mbalimbali za ubunifu zinazoendeshwa katika kituo hicho. Rais Dkt. Mwinyi pia ametembelea IITM Pravartak Technologies Foundation, kitovu cha uvumbuzi wa teknolojia kinachohusishwa na IIT Madras, ambacho kinaendeleza tafiti, ujuzi na suluhisho za kiteknolojia katika maeneo ya akili mnemba, mifumo ya mawasiliano, usalama wa …