POLISI YACHUKUA SAMPULI ZA DEREVA WA HECHE KUBAINI CHANZO CHA KIFO CHAKE

POLISI YACHUKUA SAMPULI ZA DEREVA WA HECHE KUBAINI CHANZO CHA KIFO CHAKE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma kupitia kwa Kamanda wa Mkoa huo Philimon Makungu, limesema uchunguzi wa kisayansi kuhusu kifo cha mwanachama wa CHADEMA na aliyekuwa Dereva wa John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Suezi Dani Maradufu, unaendelea huku sampuli mbalimbali zikichukuliwa kwaajili ya uchunguzi zaidi ili kuthibitisha chanzo halisi cha kifo chake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma leo Ijumaa Julai 3, 2026, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kisayansi na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Bugando pamoja na wataalamu kutoka mikoa ya Geita na Dodoma, wakishirikiana na Afisa Mwandamizi kutoka Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Uchunguzi huo umefanyika mbele ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ndugu wa marehemu. Polisi wamesema baada ya uchunguzi huo, sampuli zimechukuliwa kwaajili ya uchunguzi wa kina zaidi wa kisayansi ili kuthibitisha chanzo halisi cha kifo, na kwamba matokeo yatakapokamilika yataisaidia…