NAIBU WAZIRI MAHUNDI: MALEZI BORA NI UWEKEZAJI WA KIZAZI NA MAENDELEO YA TAIFA
NAIBU WAZIRI MAHUNDI: MALEZI BORA NI UWEKEZAJI WA KIZAZI NA MAENDELEO YA TAIFA Na Jackline Minja, WMMJW Mtwara Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesisitiza umuhimu wa malezi na makuzi bora kwa watoto, akieleza kuwa ndiyo msingi wa kujenga kizazi chenye maadili, afya njema, elimu na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na Taifa. Akizungumza katika nyakati tofauti tarehe 1Julai, 2026 mkoani Mtwara, Naibu Waziri Mahundi amesema malezi ya mtoto ni jukumu la wazazi wote wawili, hivyo akawataka akina baba na akina mama kushirikiana kwa karibu katika kuwalea watoto wao badala ya kumwachia mzazi mmoja jukumu hilo. “Malezi ya mtoto si jukumu la mama pekee, Baba na mama wanapaswa kushirikiana kwa upendo, uwajibikaji na mshikamano ili kuwajengea watoto msingi imara wa maisha kwa kuwa watoto wa leo ndiyo viongozi na nguvu kazi ya kesho, hivyo wanahitaji kulelewa katika mazingira salama na yenye maadili mema,” amesema Naibu Waziri Mahundi. Aidha, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inae…