MWENYEKITI WAZAZI TAIFA AKEMEA TABIA YA BAADHI YA VIONGOZI PWANI KUPANGA SAFU KATIKA UCHAGUZI

MWENYEKITI WAZAZI TAIFA AKEMEA TABIA YA BAADHI YA VIONGOZI PWANI KUPANGA SAFU KATIKA UCHAGUZI
Na Victor  Masangu, Bagamoyo  Mwenyekiti wa Jumuiya ya  ya Wazazi Taifa Ndg. Fadhili Maganya amekemea vikali baadhi  viongozi wa CCM wakiwemo madiwani na wabunge kuachana na vitendo vya kupanga safu hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2027. Hayo ameyabainisha  wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kukiimarisha chama pamoja na jumuiya zake zote ikiwa samba samba na kuangalia uhai wa chama. “Kitu kikubwa ninachowaomba viongozi,madiwani pamoja na wabunge  kuondokana kabisa na masuala ya kuamua kupanga safu kabla ya uchaguzi lkn kitu kikubwa wanaotaka kugombea ruksa kugombea nafasi mbali mbali,”amesema Mwenyekiti huyo. Pia amefafanua kwamba mwakani ni kipindi cha uchaguzi hivyo hakusita kuwaasa wanachama wote kuanzia ngazi za mashina wasisite kujitokeza katika kugombea nafasi mbali mbali. Kadhalika ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kuweza kusimamia vizuri utekelezaji wa ilani na ukusanyaji wa fedha za mapato ya ndani ambazo zimekwenda kutekeleza miradi ya m…