MVOMERO WAPOKEA BILIONI 1.1 ZA KUJENGA SHULE MBILI

MVOMERO WAPOKEA BILIONI 1.1 ZA KUJENGA SHULE MBILI
•Prof. Shemdoe atoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za watumishi Na. OWM–TAMISEMI, Mvomero Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wananchi wa mvomero la kujengewa shule mbili za Sekondari katika Halmashauri ya Mvomero, ombi ambalo liliwasilishwa kwa niaba yao na Mbunge wa Jimbo la Mvomero Mhe. Sara Msafiri pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Josephine Kapoma wakilenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji katika Halmashauri hiyo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Julai 18, 2026 katika kijiji cha Mkindo, kata ya Mkindo, Halmashauri ya Mvomero Mkoa wa Morogoro, mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika miradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkindo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi w…