MHE BALOZI OMAR: MAPINDUZI YA VIWANDA NI MUHIMU KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI ZA AFRIKA
MHE BALOZI OMAR: MAPINDUZI YA VIWANDA NI MUHIMU KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI ZA AFRIKA Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa akishiriki mjadala kuhusu nafasi ya sekta ya viwanda inavyoweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi Afrika, mjadala uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa African Caucus wa Mwaka 2026, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia, ambapo amesema kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuchukua hatua madhubiti za kisera na kikodi ili kuiwezesha sekta ya viwanda kuchangia ukuaji wa uchumi, kukuza ajira, kuimarisha uzalishaji na kupanua mauzo ya nje. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Banjul, Gambia) ………….. Na Benny Mwaipaja, Banjul, Gambia. Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuchukua hatua madhubiti za kisera na kikodi ili kuiwezesha sekta ya viwanda kuchangia ukuaji wa uchumi, kukuza ajira, kuimarisha uzalishaji na kupanua mauzo ya nje. Mhe. Balozi Omar amesema hayo aliposhiriki mjadala kuhusu nafasi ya…