MBUNGE LUTEVELE WA MAFINGA MJINI AIOMBA SERIKALI KUHARAKISHA UJENZI WA BARABARA YA MAFINGA–MGOLOLO
MBUNGE LUTEVELE WA MAFINGA MJINI AIOMBA SERIKALI KUHARAKISHA UJENZI WA BARABARA YA MAFINGA–MGOLOLO NA DENIS MLOWE, MUFINDI MBUNGE wa Jimbo la Mafinga Mjini, Dickson Lutevele, ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mafinga–Mgololo akisema ni kiungo muhimu cha uchumi wa Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla. Lutevele alisema licha ya barabara hiyo kuonekana kupitika wakati wa kiangazi, kipindi cha masika hali huwa ngumu na kuathiri usafirishaji wa mazao, mbao na bidhaa nyingine zinazochangia uchumi wa eneo hilo. Akizungumza mbele ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, Lutevele alisema wananchi wa Mafinga Mjini wanategemea kwa kiasi kikubwa shughuli za uzalishaji zinazofanyika maeneo ya vijijini, hivyo kuboreshwa kwa miundombinu hiyo kutaimarisha biashara na kuongeza fursa za kiuchumi. Alisisitiza kuwa wabunge wa Mkoa wa Iringa wamekuwa wakizungumza kwa pamoja kuhusu umuhimu wa mradi huo bungeni na kuomba Serikali ianze utekelezaji wake bila kuchelewa. Akijibu ombi hilo, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtuma kuwasalimu wananchi …