MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA OACPS
MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA OACPS Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki, mazungumzo yaliyofanyika Jijini Arusha. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki, mara baada ya mazungumzo, yaliyofanyika Jijini Arusha. …………….. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki, mazungumzo yaliyofanyika Jijini Arusha. Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amemuhakikishia Katibu Mkuu wa OACPS dhamira ya Tanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kuleta mageuzi na kuifanya kuwa na tija kwa nchi wanachama. Aidha amempon…