MAANDALIZI YA KUPOKEA MWENGE WA UHURU YAKAMILIKA ARUSHA, ALI KIBA NA JUMA NATURE KUPAMBA MKESHA

MAANDALIZI YA KUPOKEA MWENGE WA UHURU YAKAMILIKA ARUSHA, ALI KIBA NA JUMA NATURE KUPAMBA MKESHA
Na Pamela Mollel,Arusha  Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Arusha yamekamilika kwa asilimia 100, huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za Mbio za Mwenge, kutembelea miradi ya maendeleo na kuhudhuria mkesha mkubwa wa burudani utakaofanyika Viwanja vya FFU Mworombo jijini Arusha  Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, anasema maandalizi yote yamekamilika na wilaya ipo tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru, huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu Anasema Mwenge wa Uhuru utatembelea na kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha maendeleo na kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wananchi Mkude anasema mbali na miradi ya maendeleo, Mwenge wa Uhuru utaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya UKIMWI, malaria, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na utunzaji wa mazingira kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu ise…