KATIBU WA UWT TAIFA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA KUAGA MWILI WA BALOZI JUMA SAIGWA MACHAKA DODOMA

KATIBU WA UWT TAIFA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA KUAGA MWILI WA BALOZI JUMA SAIGWA MACHAKA DODOMA
Na Barnabas Kisengi, Dodoma Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kushiriki ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Balozi Juma Saigwa Machaka, aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mjumbe wa Shina Na. 5, Tawi la Kilimani, jijini Dodoma. Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Anglican-Chinyoyo, Kata ya Kilimani, na kuongozwa na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Suzani Kunambi, ambaye aliambatana na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pilli Mbaga, pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali. Akitoa salamu za rambirambi, Suzani Kunambi alisema CCM imepoteza kiongozi mwenye uadilifu, mzalendo na mtumishi aliyekuwa akijitoa kwa dhati katika kutumikia chama, jamii na Taifa. Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pilli Mbaga, alisema marehemu Juma Saigwa Machaka alikuwa mfano wa uongozi wa karibu na wananchi, akihakikisha usalama na mshikamano wa wanachama katika eneo lake. "Tukianza kueleza sifa za Balozi Juma Saigwa Machaka hatutamaliza. Alikuwa mwadilifu, mzalendo …