KABUDI AIPONGEZA DCEA KWA ELIMU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA SABASABA,
KABUDI AIPONGEZA DCEA KWA ELIMU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA SABASABA,
-Awahimiza wananchi kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa juhudi zake za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Prof. Kabudi alitoa pongezi hizo Julai 4, 2026, alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo pia aliwahimiza wananchi kutembelea banda hilo ili kujipatia elimu, ushauri wa kitaalamu na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo. Akiwa katika banda hilo, Prof. Kabudi alijionea shughuli zinazotekelezwa na taasisi mbalimbali, ikiwemo DCEA, ambayo inaendelea kutoa elimu ya kinga dhidi ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na madhara yake kwa jamii. Alisema Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu li…