Global kufanya maonesho ya elimu Mwanza kesho

Global kufanya maonesho ya elimu Mwanza kesho
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar GLOBAL Education Link (GEL) imesema jumla ya wanafunzi, wazazi na walezi 1,113 wamefikiwa na kupatiwa huduma kupitia maonesho ya Global Education Fair 2026 yaliyofanyika Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam na leo Jumanne yanafanyika Four Point by Sheraton Arusha na tarehe 30 Rockcity Mall Mwanza. Akizungumza baada ya kukamilika kwa maonesho yaliyofanyika Julai 25, 2026 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmalik Mollel, alisema mwitikio huo unaonesha kuongezeka kwa uhitaji wa taarifa sahihi kuhusu fursa za kusoma nje ya nchi. Alisema kupitia maonesho hayo, washiriki walipata ushauri kuhusu uchaguzi wa kozi, vyuo vikuu, scholarships, gharama za masomo, malazi, visa na maisha ya mwanafunzi katika mataifa mbalimbali. “Mwitikio tulioupata Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam unaonesha kuwa wanafunzi na wazazi wanahitaji mwongozo sahihi kabla ya kufanya maamuzi kuhusu elimu ya juu,” alisema Bwana Mollel. Alisema zaidi ya watu 700 w…