Dkt. Mwigulu Nchemba Aongoza Washiriki Zaidi ya 13,000 NBC Dodoma Marathon; Shilingi Bilioni 1 Zakusanywa Kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto

Dkt. Mwigulu Nchemba Aongoza Washiriki Zaidi ya 13,000 NBC Dodoma Marathon; Shilingi Bilioni 1 Zakusanywa Kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo ameongoza zaidi ya washiriki 13,000 katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2026 zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku akiipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kufanikisha ukusanyaji wa shilingi bilioni 1 zitakazotumika kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia miradi ya afya ya mama na mtoto. Fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa maeneo matatu muhimu ya kijamii ambayo ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua, kugharamia upasuaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, pamoja na kuimarisha huduma za upandikizaji wa uloto kwa watoto wanaoishi na ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell). Mbio hizo, ambazo zimeendelea kujijengea hadhi kama moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo nchini, zilihusisha washiriki kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali, huku zikishuhudia ushindani mkubwa kati ya wanariadha wa Tanzania na Kenya katika mbio za kilomita 21 na 42. Dkt. Nchemba, pamo…