DIWANI AENDELEA KUCHANGIA CHAKULA KWA WANAFUNZI

DIWANI AENDELEA KUCHANGIA CHAKULA KWA WANAFUNZI
Na George Maziku, Kahama DIWANI wa Kata ya Majengo, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga Shida Zacharia Soko amechangia chakula chenye thamani ya zaidi ya milioni 6 kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma kwenye shule tatu zilizopo kwenye kata yake. Chakula hicho amekitoa juzi katika mkutano wa wazazi wa wanafunzi wanaosoma katikà shule tatu za Mama Samia Sekondari, shule ya msingi Anderson Msumba na shule ya msingi Majengo. Mkutano huo aliuitisha yeye mwenyewe kwa lengo la kuwahasisha wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda.  Diwani huyo alitoa gunia 45 za mahindi yenye thamani ya milioni 2925000, maharage kilogramu 600 zenye thamani ya Sh. milioni 1200000, Mchele kilogramu 600 zenye thamani ya 12000, na sukari kilogramu 600  zenye thamani ya Sh. 1200000. Akitoa mchanganuo wa mchango huo wakati akiukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya, diwani Soko alisema kila shule itapata gunia 15 za mahindi, kilo…