DCEA: UCHEPUSHWAJI WA DAWA TIBA HUCHOCHEA URAIBU, UHALIFU NA MADHARA YA KIAFYA
DCEA: UCHEPUSHWAJI WA DAWA TIBA HUCHOCHEA URAIBU, UHALIFU NA MADHARA YA KIAFYA Matumizi mabaya ya dawa tiba zenye asili ya kulevya yameelezwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochochea ongezeko la uraibu, uhalifu na athari mbalimbali za kiafya pale dawa hizo zinapochepushwa kutoka katika matumizi yake halali ya kitabibu na kutumiwa kutengeneza au kuchanganywa na dawa za kulevya. Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi wa Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Ziliwa Peter Machibya, wakati akiwasilisha mada katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho, jijini Dar es Salaam, Julai 3, 2026. Machibya amesema ni muhimu jamii kutambua kuwa dawa tiba zenye asili ya kulevya si dawa za kulevya zenyewe, bali ni dawa halali zinazotumika katika huduma za afya kwa madhumuni ya matibabu chini ya usimamizi wa wataalamu wa afya. Amesema tatizo huanza pale dawa hizo zinapochepushwa kutoka kwenye matumizi yake halali na kutumiwa kutengeneza au kuchanganywa na dawa za kulevya. “Dawa tiba zenye asili ya kulevya si dawa …