BARRICK-TWIGA, SERIKALI WAZINDUA AWAMU YA PILI YA MRADI WA BARRICK FUTURE FORWARD EDUCATION PROGRAM

Na Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma Kampuni ya Barrick inayofanya shughuli zake kwa ubia na Serikali kupitia Twiga Minerals imeahidi kuwa kupitia programu ya Barrick-Twiga Future Forward Education Program itaendelea kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuimarisha miundombinu na kuwezesha mazingira rafiki ya kujifunzia ili kuchochea maendeleo ya taifa. Akizungumza Julai 2,2026 na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa kitaifa wa awamu ya pili ya mradi huo, Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido, amesema kuwa baada ya makubaliano na Serikali mwaka 2023, Barrick ilikubali kutoa zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule za sekondari nchini. Amesema kuwa mradi wa Barrick-Twiga Future Forward Education Program unalenga kuwekeza kwa Watanzania kwa kuweka mbele maslahi ya jamii kupitia uboreshaji wa miundombinu ya elimu ili kutengeneza mazingira bora zaidi ya kujifunza …