UVCCM SHINYANGA: TUSIHANGAIKE NA MATUSI YA WAPINZANI MTANDAONI, TUWAJIBU KWA MATOKEO YA KAZI
UVCCM SHINYANGA: TUSIHANGAIKE NA MATUSI YA WAPINZANI MTANDAONI, TUWAJIBU KWA MATOKEO YA KAZI
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026. Picha na Kadama Malunde Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga imewataka vijana wake kuendelea kulinda amani, kujiepusha na mijadala ya matusi kwenye mitandao ya kijamii na badala yake kujikita katika kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kama njia bora ya kujibu hoja za wapinzani. Wito huo umetolewa leo Juni 24, 2026 na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo amesi…