TURACO COLLECTION YANG’ARA KARIBU-KILIFAIR 2026, YAISIFU TANZANIA KIMATAIFA

TURACO COLLECTION YANG’ARA KARIBU-KILIFAIR 2026, YAISIFU TANZANIA KIMATAIFA
Na Mwandishi Wetu, Arusha MKURUGENZI wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata, amesema maonesho ya Karibu-KiliFAIR 2026 ni jukwaa muhimu la kuitangaza Tanzania kimataifa, kubadilishana uzoefu pamoja na kujenga ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya utalii inayokua kwa kasi duniani. Akizungumza wakati akiwasilisha hoteli za Turaco Collection katika maonesho hayo yanayofanyika jijini Arusha, Florenso alisema tukio hilo limekuwa likiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, ukarimu, safari na uwekezaji kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali duniani. Maonesho ya Karibu-KiliFAIR 2026 yanafanyika kuanzia Juni 4 hadi 7, 2026 katika Viwanja vya Magereza jijini Arusha. Florenso alisema Turaco Collection imeendelea kuimarisha uwepo wake nchini kupitia hoteli zake zilizopo katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Alitaja hoteli hizo kuwa ni pamoja na Element by Westin Dar es Salaam na Delta Hotels by Marriott Dar es Salaam zilizopo Dar es Salaam. Aidha, alisema Kaskazini mwa T…