TRA MKOA WA PWANI YAMWAGA VIFAA KWA MAMA LISHE NA WALIPA KODI CHALINZE
TRA MKOA WA PWANI YAMWAGA VIFAA KWA MAMA LISHE NA WALIPA KODI CHALINZE
Na Victor Masangu, Pwani Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 imeamua kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na walipa kodi kwa kufanya usafi katika stendi ya mabasi chalinze pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya usafi kwa wafanyabiashara pamoja na kutoa vyombo mbali mbali vya kupikia kwa wakinamama ambao ni mama lishe. Katika msafara huo ambao uliongozwa na Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Zanzibar Salehe Haji Pandu amesema kwamba wameamua kwenda kuwatembelea wafanyabiashara wa chalinze kwa lengo la kuweza kuwasaidia ili waweze kuhakikisha wanapiga hatua katika kutimiza ndoto zao. "Katika kuelekea katika maadhimisho ya miaka 30 ya TRA tumeamua kwenda kufanya usafi katika stendi ya Chalinze ikiwa pamoja kugawa vifaa vya Usafi pamoja na Vyombo vya kupikia kwa Mama lishe pamoja na kuwawatembelea wafanyabiashara wa stendi ya Chalinze katika kutambua mchango wao kwa walipa kodi,"amebainisha Kamishna …