TASAC Yaahidi Kuendelea Kuimarisha Viwango na Usalama wa Mabaharia

TASAC Yaahidi Kuendelea Kuimarisha Viwango na Usalama wa Mabaharia
Na Mwandishi Wetu, Kigoma Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mohamed Salum, amesema mabaharia wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa kutokana na nafasi yao muhimu katika usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka nchini. Salum aliyasema hayo wakati akifungua  Warsha  kuelekea kilele cha Maadhomisho  cha Siku ya 16 ya Mabaharia Duniani yanayofanyika mkoani Kigoma, ambapo alieleza kuwa takribani asilimia 80 ya bidhaa zinazoingia nchini husafirishwa kwa njia ya maji na kufikishwa kwa watumiaji kupitia juhudi za mabaharia. Alisema mchango wa mabaharia hauishii kwenye usafirishaji wa bidhaa pekee, bali pia una athari kubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuhakikisha mnyororo wa biashara unaendelea kufanya kazi kwa ufanisi. “Mabaharia ni nguzo muhimu ya uzalishaji na maendeleo ya uchumi. Bila wao, shughuli nyingi za biashara na usafirishaji zingekwama,” alisema Salum. Aliongeza kuwa TASAC itaendelea kusimamia na kuratibu sekta ya mabaharia…