TANROADS: ULINZI WA MIUNDOBINU YA BARABARA NA MADARAJA NI JUKUMU LA KILA MWANANCHI

TANROADS: ULINZI WA MIUNDOBINU YA BARABARA NA MADARAJA NI JUKUMU LA KILA MWANANCHI
📌 Kamera Kufungwa Kudhibiti Uharibifu Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kigoma imetoa rai kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa miundombinu ya barabara kushiriki kikamilifu katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwa salama kwa watumiaji. Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Elsony Mweladzi, ambaye amesema kuwa mkoa huo una jumla ya madaraja 396, yakiwemo madaraja makubwa matano ambayo yote yako katika hali nzuri na salama kwa matumizi ya wananchi. Mhandisi Mweladzi amesema ni muhimu wananchi kutunza na kulinda uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika miundombinu ya barabara na madaraja ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na vitendo vya uharibifu. “Niwasihi wananchi wanaoishi maeneo yanayopitiwa na barabara, hususan eneo la Malagarasi katika Daraja la Kikwete, kutunza miundombinu iliyowekwa ikiwemo taa za barabarani kwa kuepuka kuzihujumu na hivyo kuisab…