TAKUKURU RUKWA YAWAJENGEA UWEZO WASIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO KUOKOA FEDHA ZA WANANCHI
TAKUKURU RUKWA YAWAJENGEA UWEZO WASIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO KUOKOA FEDHA ZA WANANCHI
Jane Mwakyoma, Juni 25, 2026, Rukwa. TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Rukwa imeendesha mafunzo maalumu kwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo kutoka halmashauri zote nne za mkoa huo, yakilenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa miradi. Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amewataka wasimamizi wa miradi kutumia elimu wanayopewa kama nyenzo ya kuimarisha usimamizi wa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Amesema utekelezaji wa miradi bila kuzingatia sheria, kanuni za manunuzi na taratibu za ujenzi unaweza kusababisha migogoro hasara kwa Serikali na kuchelewesha huduma muhimu zinazotarajiwa na wananchi. “Miradi ya maendeleo ni matumaini ya wananchi. Ni wajibu wa kila msimamizi kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa uadilifu na miradi inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati,” amesema. Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU Mko…