SERIKALI YAENDELEA KUCHUKUA HATUA KUIMARISHA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KWA WATOTO
SERIKALI YAENDELEA KUCHUKUA HATUA KUIMARISHA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KWA WATOTO Na Jackline Minja, WMJWM Dodoma Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuratibu vikao shirikishi vya kijamii vinavyowapa elimu wazazi na walezi kuhusu wajibu wao wa malezi, matunzo na ulinzi wa watoto, hususan yatima na watoto wenye ulemavu. Hayo yameelezwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Bungeni jijini Dodoma leo, Juni 26, 2026, alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge. Waziri Dkt. Gwajima amewataka wazazi kutoruhusu migogoro yao ya kifamilia kuwa chanzo cha watoto kukosa malezi na kuishia kuishi mitaani katika mazingira hatarishi. “Wazazi niwasihi pale ambapo migogoro ya wazazi itakuwa imefikia hatua ya kushindwa kuwalea watoto kwa wakati, ni vyema mkakawapeleka watoto hao katika vituo vya ustawi wa jamii ili wapate malezi na ulinzi stahiki kwa muda, badala ya kuwaacha wakitelekezwa.” amesema Dkt. Gwajima Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Msalala, M…