OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAPOKEA UJUMBE WA UBALOZI WA JAPAN

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepokea Ujumbe na kufanya mazungumzo kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania. Ujumbe huo umetembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyoko Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 9 Juni, 2026.  Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Kisheria Ndani ya Serikali, Bw. Ipyana Mlilo amesema kuwa lengo la ujumbe huo ni kuaga pamoja na kumtambulisha Mratibu mpya ambaye atakuwa anashughulia ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ubalozi huo. Alitumia fursa hiyo kushukuru Ubalozi huo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuomba kuendeleza ushirikiano huo hasa katika mafunzo ya kisheria. Ujumbe huo uliongozwa na Mratibu anayemaliza muda wake, Bi. Yoshino Shibata ambaye alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa ushirikiano mkubwa na wa kihistoria waliompa katika kipindi chote cha utumishi wake nchini. Kwa upande wake, Fum…