NDALLU- WANACHAMA WAPYA 165 WAJIUNGA UWT KIBAHA MJINI

NDALLU- WANACHAMA WAPYA 165 WAJIUNGA UWT KIBAHA MJINI
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WANACHAMA wapya 165 wamejiunga na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kibaha Mjini, Mkoa wa Pwani, hatua inayoonesha mwitikio wa wanawake kushiriki katika umoja huo. Wanachama hao wametoka katika kata tatu, ambapo Tumbi wamejiunga wanachama 65, Kongowe 50 na Maili Moja 50. Katibu wa UWT Kibaha Mjini, Cecilia Ndallu, anaeleza kuwa kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, idadi ya wanachama wa jumuiya hiyo ilikuwa imefikia 35,844, hivyo baada ya ongezeko la wanachama hao 165 idadi itafikia 36,009. Aidha ameeleza UWT Kibaha Mjini imefanikiwa kujenga ofisi katika kata tano kati ya kata 14 zilizopo, hatua inayolenga kuimarisha utendaji kazi wa jumuiya hiyo. Vilevile amewahimiza wanawake wengine kuendelea kujiunga na umoja huo ili kuwa sehemu ya jukwaa la kushirikiana, kujifunza na kushiriki katika shughuli za maendeleo. Ndallu amewataka wanachama kulipa ada kwa wakati, huku akiwaomba kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kueleza mafanikio ya mageuzi makubwa …