MWIJAGE CUP YAZINDULIWA KAMACHUMU, TIMU 20 ZASHINDANIA SHILINGI MILIONI 6
MWIJAGE CUP YAZINDULIWA KAMACHUMU, TIMU 20 ZASHINDANIA SHILINGI MILIONI 6 Na Silivia Amandius Muleba,Kagera. Mashindano ya soka kwa vijana ya Kamachumu Paul Mwijage Cup yamezinduliwa rasmi katika Tarafa ya Kamachumu, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, yakishirikisha timu 20 zinazowania zawadi ya shilingi milioni 6 kwa lengo la kuibua vipaji na kukuza maendeleo ya michezo katika jamii. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika Juni 7 katika Uwanja wa Polisi Kamachumu, Ndg. Paul Mwijage, amesema kuwa ligi hiyo inapaswa kuwa desturi ya kuwakutanisha vijana mara kwa mara ili pamoja na michezo waweze kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayowahusu. Mwijage amesema kuwa mashindano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya taasisi yake ya Mwijage Compassion and Development Foundation, ambayo inalenga kuanzisha akademi za michezo zitakazosaidia kukuza vipaji vya vijana. Ameeleza kuwa kuanzia Kamachumu ni hatua ya kuwapa nafasi vijana wenye umri chini ya miaka 20 kuonesha uwezo wao na kufungua fursa za maendeleo kupitia michezo. Aidha, amesema a…